Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/21/2015 8:57:58 PM
Maandalizi ya sikukuu ya wafanyakazi mkoa wa Pwani yameanza ambayo mwaka huu kimkoa yatafanika wilayani Mafia chini ya usimamizi wa chama cha wahifadhi,mahoteli na nyumba za kulala wageni.
Mwenyekiti wa CHODAWU Mkoa wa PWANI, BW.PIUS MSILU amesema mwaka huu maadhimisho hayo yanafanyika wilayani Mafia ili kutoa fursa kwa wafanyakazi kisiwani humo kushiriki kikamilifu sherehe hizo na kuweza kuweka bayana changamoto mbalimbali zinazowakabili.
BW.MSILU ameongeza kuwa wamejipanga kuhakikisha wanawasiliana na waajiri na wadau wengine katika kuhakikisha wanapata fedha za kutosha kufanikisha maadhimisho hayo.
Ameongeza kuwa ni wajibu wa waajiri kuwasilisha majina ya wafanyakazi bora ili waweze kupatiwa zawadi wanazostahili, ameongeza kuwa CHODAWU imepata mafanikio mbalimbali kwa kuwasaidia wafanyakazi wanachama wa chama hicho kupata haki zao msingi.
Naye mjumbe wa CHODAWU kutoka Wilayani Mafia BW.CLEVER MWAIKAMBO amewataka watu wote watakaoshiriki maadhimisho hayo kutumia fursa hiyo kuja kuyafahamu mazingira ya kuvutia ya kisiwa hicho chenye utajiri mkubwa mazao ya bahari.
END.
VSP Group, my partner program. Get connected! https://youpartnerwsp.com/en/join?72003
Мы используем cookie-файлы, чтобы улучшить сервисы для вас. Если ваш возраст менее 13 лет, настроить cookie-файлы должен ваш законный представитель. Больше информации